Featured

    Featured Posts

SERIKALI YAKUBALI OMBI LA MBUNGE MASARE KUJENGA MALAMBO ITIGI+video

 Na Richard Mwaikenda, Dodoma

Mbunge wa YAHAYA OMARI MASARE wa Jimbo la Manyoni Magharibi amepambana bungeni kuhakikisha serikali inakubali kujenga malambo kwa ajili ya wafugaji kunywesha mifugo yao maji.kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Itigi.Masare amehoji bungeni kuwa ni lini serikali itajenga malambo hayo ambapo Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Mdaki alikuwa na majibu yafuatayo;:-Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mhe. Yahaya Omari Masare –(Manyoni Magharibi ) kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, inategemea ifikapo2025, itaongeza idadi ya malambo na mabwawa ya maji ya mifugo kutoka 1,384 hadi1,842 na visima virefu kutoka 103 hadi 225. Aidha, katika mwaka wa fedha 2020/2021,Wizara inakamilisha ujenzi wa mabwawa matatu ya Chamakweza (Chalinze),Kimokouwa (Longido) na Narakauo (Simanjiro) pamoja na ujenzi wa visima virefu viwilicha Usolanga, (Iringa D.C) na Mpapa (Manyoni D.C).Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa 2021/2022, Wizara imepanga kutekeleza ujenziwa mabwawa matano (5) yenye thamani ya shilingi bilioni 1.6 na visima virefu sita(6) vyenye thamani ya shilingi milioni 560 kwa maeneo yenye changamoto ya ukamena uhitaji mkubwa wa maji nchini. Wizara itaangalia uwezekano wa kuingizaHalmashauri ya Itigi katika mpango kutegemeana na Bajeti.Mheshimiwa Spika, nitoe rai kwa Waheshimiwa Wabunge, Madiwani na Wakurugenzikatika halmashauri zetu, ikiwemo Halmashauri ya Itigi, kutenga na kutumia asilimia 15ya mapato ya ndani yatokanayo na mifugo kujenga miundombinu muhimu kwa mifugo,ikiwa ni pamoja na mabwawa, majosho, malambo, visima, minada n.k.Pia, Waziri amekubali ombi la Mbunge Masare kuambatana naye jimboni kwenda kujionea hali halisi ya changamoto ukosefu wa malambo kwa ajili ya kunyweshea maji mifugo.Mdau nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Mbunge Masare akiuliza na Waziri Mdaki akijibu... Imeandaliwa na Richard Mwaikenda Mhariri Blog ya Taifa ya CCM 0754264203
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana