Featured

    Featured Posts

WAZIRI UMMY AFANYA ZIARA STENDI KUU DODOMA AAGIZA KUBADILISHWA KWA MFUMO WA UENDESHAJI WAKE.

 


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu, akizungumza Leo April 12,2021 wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa mradi wa kituo kikuu cha mabasi cha nane nane Jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge wa kwanza kulia akitolea ufafanuzi jambo wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu, alipotembelea kukagua utendaji kazi wa mradi wa kituo kikuu cha mabasi nanenane leo April 12,2021 jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa jiji la Dodoma bw. Joseph Mafuru akitolea ufafanuzi jambo wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu, alipotembelea kukagua utendaji kazi wa mradi wa kituo kikuu cha mabasi nanenane leo April 12,2021 jijini Dodoma.

Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Antony Mavunde akizungumza  wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu, alipotembelea kukagua utendaji kazi wa mradi wa kituo kikuu cha mabasi nanenane  leo April 12,2021 jijini Dodoma.

Meneja wa kituo kikuu cha mabasi cha nanenane jijini Dodoma bw. Abedi Msangi, akitolea ufafanuzi jambo wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu, alipotembelea kukagua utendaji kazi wa mradi wa kituo kikuu cha mabasi nanenane  leo April 12,2021 jijini Dodoma.

………………………………………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu ameliagiza Jiji la Dodoma kuunda chambo maalumu kwa ajili ya uendeshaji wa miradi mikubwa ya kimkakati waliyonayo na sio mfumo wa sasa ambapo miradi inaendeshwa na jiji kama kituo hicho kikuu cha mabasi.

Pia ametaka mfumo huo uwe rafiki kwa  wateja, wajasiliamali pamoja na wafanyabiashara wa usafirishaji na sio kituo hicho kugeuka kero kwa wananchi pindi wanapopata huduma.

Waziri Ummy ametoa maagizo hayo leo April 12, 2021 wakati alipofanya ziara katika kituo kikuu cha mabasi nanenane, kilichopo katika jijini la Dodoma, ambapo amesema lazima kiundwe chombo kwa ajili ya kuendesha miradi hiyo ili iweze kuleta tija kwa nchi kama malengo yalivyokusudiwa.

“Kuna muongozo maalumu wa uendeshaji wa miradi hii, ili ilete tija, mimi nadhani kiundwe chombo maalumu cha kuendesha miradi hii ili tufikie lengo tulilokusudia, tunataka miradi hii izalishe mapato ili tukajenge shule, hospitali” amesema Waziri Ummy.

Amesema Serikali imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 24 katika mradi huo wa stendi hivyo mradi huo usimamiwe kikamilifu ili itolewe huduma bora, huku akitaka mabasi yote yaanzie na kumalizia safari zake katika kituo hicho.

Amesema serikali ya awamu ya sita itaendelea kujali wafanyabiashara wadogo wadogo na kusema kama alivyoruhusu hayati Dkt John Magufuli kuwa wajasiliamali kufanya biashara katika kituo hicho ndivyo itakavyokuwa na kutaka wafanyebiashara zao kwa amani na kwa kufuata sheria.

Kwa upande wake meneja wa kituo kikuu cha mabasi nanenane bwana Abedi Msangi amesema kituo hicho kilianza kutoa huduma juni 8, 2020 na kinauwezo wa kuhudumia mabasi mia moja (100) kwa wakati mmoja, na mpaka sasa tayari wameshakusanya shilingi milioni mia sita themanini (680) katika shughuli zake.

Amesema walikusudia kukusanya zaidi ya shilingi bilioni mbili mpaka sasa lakini wamekusanya shilingi milioni mia sita na themanini kutokana na mwitikio hafifu wa wafanyabiashara na wengine kuchukua vizimba na kutoanza shughuli katika kituo hicho.

Ameongeza kuwa “kutokana na changamoto hii tumeamua kushusha kodi ya pango kutoka kodi ya awali ya shilingi elfu 15 kwa squre mita hadi kufikia elfu kumi (10000) kwa aqure mita ili tuwavutie wateja kuanza kufanya biashara” amesema Msangi.

Nae Mkurugenzi wa jiji la Dodoma bwana Joseph Mafuru amesema mpaka sasa mradi huo unasimamiwa na jiji lakini wapo katika mchakato kuendesha kwa mfumo mwingine na wameshapeleka andiko ofisi ya Mkoa ili kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa mradi huo na miradi mingine iliyopo katika jiji la Dodoma.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana