Featured

    Featured Posts

IGP SIRRO AMVALISHA CHEO CHA UKAMISHNA, KAMISHNA MTEULE SALUM HAMDUNI

 

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro (kulia) akimvalisha cheo Kamishna Msaidizi wa Polisi Salum Hamdun kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, baada ya Mhe. Rais kumpandisha cheo kuwa kamishna wa Jeshi la Polisi. Hafla hiyo imefanyika leo Makao Makuu ndogo ya Polisi jijini Dar es salaam.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akimkabidhi Kamishna wa Polisi CP Salum Hamdun, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kitabu cha Muongozo kinacholiongoza Jeshi la Polisi baada ya kumvalisha Cheo cha Ukamishna kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, baada ya Mhe. Rais kumpandisha Cheo kuwa Kamishna wa Jeshi la Polisi. Hafla hiyo imefanyika leo Makao Makuu ndogo ya Polisi jijini Dar es salaam.

Picha na Jeshi la Polisi

…………………………………………………………………………..

 DAR ES SALAAM

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amemtaka kamishna Salum Hamdun kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa kiapo chake na kuhakikisha anasimamia sheria na taratibu za nchi ikiwa pamoja na kuwatendea haki wananchi atakaowahudumia.

IGP Sirro amesema hayo wakati akimvalisha Cheo cha Ukamishna wa Polisi CP Salum Hamdun kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan baada ya Mhe. Rais kumpandisha cheo hicho.

Hata hivyo, IGP Sirro wakati akimvalisha cheo cha Ukamishna pia alimkabidhi Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na kitabu cha muongozo kinachoongoza Jeshi hilo.

Naye Kamishna mteule CP Salum Hamduni amesema kuwa, ataendelea kutenda kazi zake kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo na kwamba atahakikisha anawatendea haki Watanzania kwa kulinda usalama wao na mali zao.

Kwa upande wake Kamishna wa Kamisheni ya Ushirikishwaji wa Jamii CP Dkt. Mussa Ali Mussa amesema kuwa, Jeshi la Polisi litaendelea kufanya kazi kwa weledi na kwa uaminifu ili kuhakikisha Jeshi linaendelea kujijengea heshima kwa wananchi.

Awali kabla ya kupandishwa cheo hicho na Mhe. Rais, Kamishna Salum Hamdun alikuwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es salaam akiwa na Cheo cha Kamishna Msaidizi wa Polisi.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana