Featured

    Featured Posts

IGP SIRRO: ATANGAZA KUANZA KWA OPERESHENI MAALUM DAR, KINONDONI YAONGOZA KWA UHALIFU

 

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, akizungumza na maafisa na askari (hawapo Pichani) wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni katika kikao kazi maalum leo tarehe 26/05/2021 ambapo amewaagiza kusimamia sheria za nchi ipasavyo na kuendelea kuwachukulia hatua kali wale wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu.

Picha na Jeshi la Polisi.

…………………………………………………………………

DAR ES SALAAM

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, ameutaja mkoa wa Kipolisi wa  kinondoni kama kinara wa uhalifu nchini ambapo matukio ya uporaji, uvunjaji wa kutumia nguvu na uporaji kwa kutumia pikipiki yakiwa yameongezeka huku uhalifu mwingine mkubwa wa kutumia silaha za moto ukiwa umeshuka.

IGP Sirro amesema hayo jijini Dar es salaam, wakati akizungumza na Wenyekiti wa Serikali za Mitaa, watendaji Kata, pamoja na watendaji wa vikundi vya ulinzi shirikishi ambapo amewataka watendaji wote kutimiza wajibu wao kwa kuhakikisha usalama unaendelea kuimarishwa.

Aidha, IGP Sirro ametoa muda wa wiki moja kuhakikisha wanakomesha vya kihalifu kwa kushirikiana na watendaji wengine huku akitoa wito kwa mgambo kuacha kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa.

Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Tegeta, Bwana Mohamed Mawala amesema kuwa, wataendelea kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia uzalendo, taratibu na kanuni na kuhakikisha maeneo yao na wananchi wanaowahudumia yanakuwa salama.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mlalakuwa Suleiman Masare, ameahidi kutoa pikipiki mpya kwa Kituo cha Polisi Chuo Kikuu itakayosaidia kurahisisha utoaji wa huduma za kipolisi kwa wananchi.

Kabla ya kukutana na watendaji wa serikali za mitaa na watendaji wa kata na watendaji wa vikundi vya ulinzi shirikishi pia IGP Sirro, alifanya kikao kazi na maofisa na askari wa Jeshi hilo ambapo aliwataka kuendelea kutimiza wajibu wao na kuwachukulia hatua kali wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana