Featured

    Featured Posts

JAMII YA WAFUGAJI MBARALI KUNUFAIKA NA MAFUNZO YA MKURABITA KUBORESHA MAISHA YAO+video

 


Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita), Anthony Temu  (wa pili kulia) akiwaelekeza maafisa wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, jinsi ya kujaza dodoso kwa kutumia mfumo wa ukusanyaji taarifa kwenye simu janja alipofanya nao kikao cha maandalizi ya kwenda kutoa mafunzo  ya kuijengea uwezo jamii ya wafugaji katika Kitongoji cha Mogelo wilayani humo. Kutoka kushoto ni Afisa Mifugo, Abbas Mubanga, Afisa Kilimo, Issa Mwambela na Afisa Ushirika, Grace Samwel.
Afisa Kilimo wa Halmashauri hiyo, Abbas Mubanga akichangia mawazo wakati wa kikao hicho. Kulia ni Afisa Ardhi, Anthony Mashilingi.
Temu akijadiliana jambo na maafisa hao.
Afisa Ardhi, Mashilingi akichangia hoja wakati wa kikao hicho cha maandalizi.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mogelo, Talas Taikoo akielezea namna Hati miliki za Kimila zilivyoinufaisha baadhi ya  jamii ya wafugaji kwa kuzitumia kama dhamana kukopa  fedha benki zilizowasaidia kununua mashamba kwa ajili ya kilimo na kusomesha  watoto wao.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mogelo, Taikoo (kulia), akiwa akizungumza na Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini, Temu pamoja na Afisa Ardhi, Mashilingi alipotembelewa nyumbani kwake Mogelo kwa lengo la kupanga maandalizi ya mafunzo hayo.
Temu akiwa ofisini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mbarali, Kivuma Msangi ambapo alijitambulisha na kumueleza jinsi mafunzo hayo yatakavyoendeshwa na kuinufaisha jamii hiyo ya wafugaji.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
 
 
JAMII ya wafugaji ambao wengi wao ni wamasai kupatiwa mafunzo na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara wa Wanyonge Tanzania (MKURABITA) ya kuwajengea uwezo kiuchumi  jinsi ya kuboresha mifugo yao na kilimo kwa kutumia hati miliki za kimila kama dhamana kukopea fedha benki na taasisi zingine za kifedha.

Akizungumza wakati wa kikao cha maandalizi ya mafunzo hayo, kilichohudhuriwa na maafisa wa Halmashauri ya Wilaya Mbarali, mkoani Mbeya, Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini wa Mkurabita, Anthony Temu amesema mafunzo hayo yanafanyika katika Kitongoji cha jamii ya wafugaji cha Mogelo kesho Mei 27,2021.

Ametaja mafunzo watakayopatiwa kuwa ni; kuboresha mifugo yao, Kanuni za kilimo bora, kuthaminisha mali zao, jinsi ya kutunza kumbukumbu za mahesabu, faida za ushirika, kuchangamkia fursa mbalimbali ikiwemo mikopo kwa kutumia hati miliki za kimila kama dhamana, faida za kujiunga na mabenki kwa ajili ya mikopo na ufugaji bora wa nyuki wa asali.

Kabla ya kikao na maofisa hao, Temu alikutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Kivuma Msangi ambapo alijitambulisha na kumueleza jinsi mafunzo hayo yatakavyoendeshwa na kuinufaisha jamii hiyo ya wafugaji.

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza clip hii ya video ujue kilichozungumzwa kuhusu maandalizi ya mafunzo hayo yatakayohudhuriwa na zaidi ya kaya 60 za jamii ya wafugaji......

Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana