"Nachingwea tumeachiwa wapwa, Wanawake wana mapengo kutokana na kipigo kutoka kwa waume zao kisa wanachelewa kurejea majumbani wakiyasaka naji takribani masaa nane mara nyingine hadi usiku wa manane," ameyasema hayo kwa uchungu na masikitiko makubwa Mbunge wa Nachingwea, Dkt Amandus Chinguile alipokuwa akichangia mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Maji bungeni Dodoma, ambapo ameiomba serikali kukamilisha haraka miradi ya maji iliyoanzishwa na kukwama ili kuwakomboa wananchi wa jimbo hilo na adha ya uhaba wa maji.
Mdau nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Mbunge Dkt Chinguile akiwapigania wananchi wa Nachingwea kupata maji...
Post a Comment