Mbunge wa Nyang'wale, mkoani Geita, Hussein Hassan ameishauri Serikali iweke mpango rasmi wa kuwakopesha wachimbaji wadogo wa madini waweze kununua zana za kisasa za uchimbaji kupunguza uharibifu wa mazingira na kuongeza kiwango cha upatikanaji wa madini kwa lengo la kuinua kipato chao pamoja na kuliingizia Taifa kipato kikubwa cha kodi.
Mbunge huyo ametoa ushauri huo wakati akichangia mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Madini bungeni Dodoma mwishoni mwa wiki.Mdau nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video ambapo pamoja na mambo mengine, Mbunge ametoa ushauri huo......Mhariri Blog ya Taifa ya CCM,0754264203
Post a Comment