Ikulu, Chamwino.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa viongozi watatu.
Taarifa iliyotolewa leo tarehe 03 Mei, 2021 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Athman Kattanga imeeleza kuwa uteuzi wa viongozi hao umetenguliwa kuanzia tarehe 30 Aprili, 2021.
Kwanza, Mhe. Rais Samia ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) Prof. Tadeo Andrew Satta.
Sambamba na hatua hiyo, Mhe. Rais Samia pia ametengua uteuzi wa wajumbe 6 wa bodi ya TASAC.
Pili, Mhe. Rais Samia ametengua uteuzi wa Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Hassan Mwang’ombe.
Tatu, Mhe. Rais Samia ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania Dkt. Harun Kondo.
Sambamba na hatua hiyo, Mhe. Rais Samia pia amevunja Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania.
Uteuzi wa viongozi watakaoshika nyadhifa hizo utafanywa baadaye.
Post a Comment