Featured

    Featured Posts

RAIS MSTAAFU WA NIGERIA OBASANJO AZUNGUMZA NA RAIS SAMIA, LEO, ATOA POLE VIFO VYA MKAPA NA DK. MAGUFULI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akiwa katika mazungumzo na Rais Mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo, Ikulu ya Chamwino, jijini Dodoma, leo.


Ikulu, Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amefanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo katika Ikulu ya Chamwino, Dodoma, leo.


Taarifa ya Ikulu imesema, katika mazungumzo hayo, Obasanjo ametoa salamu zake za rambirambi kwa Rais Samia kufuatia vifo vya waliokuwa Marais wa Tanzania Hayati Benjamin Mkapa aliyefariki Dunia Julai 23, 2020 na Hayati Dk. John Magufuli aliyefariki Dunia Machi17, 2021


Rais Mstaafu Obasanjo amempongeza Rais Samia kwa kupokea kijiti cha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na amemtakia heri katika majukumu yake.


Katika mazungumzo hayo viongozi hao pia wamezungumzia hali ya usalama Barani Afrika na umuhimu wa Wakuu wa Nchi kujadiliana na kutafuta suluhisho la migogoro hiyo ambayo inasababisha vifo vya watu wasio na hatia hasa wanawake na watoto.


Wamezungumzia pia masuala ya maendeleo hasa katika uchumi na kusisitiza umuhimu wa nchi za Afrika kuongeza ushirikiano na kuondoa vikwazo vya biashara na uwekezaji.

Rais Mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo, akizungumza na Waandishi, wakati akisindikizwa na mwenyeji wake, Rais Samia, Baada ya nazungumzo yao, leo, Ikulu ya Chamwino, jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Rais Mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo, wakati akimsindikiza mgeni wake, baada ya mazungumzo yao, Ikulu ya Chamwino, jijini Dodoma, leo.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana