Mbunge wa Busanda, mkoani Geita, Tumaini Magesa ameishauri Serikali kuanzisha Mfuko wa Wachimbaji Wadogo wa Madini kwa ajili ya kuwakopesha ili waweze kununua mitambo ya kurahisisha uchimbaji madini.
Magesa ametoa ushauri wake huo alipokuwa akichangia mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Madini bungeni Dodoma Aprili 29, 2021, ambapo pia alishauri Sekali kuongeza bajeti ya maendeleo kwenye wizara hiyo ili wananchi waweze kuona maendeleo yaliyotarajiwa. Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupita clip hii ya video, Mbunge Magesa akitoa mchango wake huo...
Post a Comment