Leo tarehe 22 Mei, 2021 Manispaa ya Ubungo imeanza kuadhimisha wiki ya huduma kwa wananchi katika eneo la Mbezi Luis, mkabala na Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli, lengo ikiwa ni kutoa elimu ya mlipa kodi, ulipaji wa ada mbalimbali pamoja na huduma za afya.
Aidha huduma mbalimbali zitatolewa ikiwemo ulipiaji wa leseni za biashara, leseni za vileo ushuru wa huduma (service levy), ushuru wa malazi,vibali vya ujenzi, vibali vya burudani na tozo mbalimbali
Pia elimu ya ufafanuzi kuhusiana na mikopo mbalimbali inayoyolewa na halmashauri itatolewa
Na zoezi la Upimaji wa afya bure , uchangiaji wa damu na kwa watoa huduma wote baba lishe, mama lishe wote mnakaribishwa.
Zifuatazo ni picha za matukio mbalimbali kuhusu mambo yalivyokuwa jana.
Post a Comment