Madiwani na Maafisa Tarafa kutoka Wilaya ya Ludewa, mkoani Njombe wakitembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma jana, kwa uratibu wa Mbunge wa Jimbo hilo, Joseph Kamonga.
Waziri wa Tamisemi, Ummy Mwalimu (kushoto) akizungumza na madiwani na maafisa Tarafa kutoka wilayani Ludewa alipokutana nao kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Ludewa ambaye aliratibu ziara hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Joseph Kamonga akijadiliana jambo na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Njombe, Balozi Pindi Chana.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Njombe, Blozi Pindi Chana akizungumza na baadhi ya madiwani na maafisa Tarafa.
Wakiwa katika picha ya pamoja
Mbunge wa Ludewa, Kamonga (kulia) akijadiliana jambo na Waziri wa Madini, Dotto Biteko wakati wa kikao na madiwani na maafisa Tarafa Ukumbi mdogo wa Msekwa kwa ajili ya kuweka mambo sawa kuhusu machimo ya Liganga na Mchuchuma yaliyopo wilayani humo.
Waziri Biteko akifafanyua jambo wakati wa kikao hicho.
Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda akizungumza wakati wa kikao na madiwani na maafisa tarafa namna ya kupata suluhu ya masoko ya mazao mbalimbali yakiwemo mahindi. Serikali imeruhusu wakulima na wafanyabiashara kuuza popote ndani na nje ya nchi.
Waziri wa Nishati, Medard Kalemani akizungumza wakati wa kikao hicoo kuhusu utatuzi wa changamoto ya umeme wilayani humo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Post a Comment