Mbunge wa Mwanga, Joseph Tadayo ameiomba Serikali kulitafutia ufumbuzi wa haraka tatizo la ukosefu wa mawasliano ya simu katika baadhi ya vijiji katika Jimbo la Mwanga kiasi cha wananchi kuingia gharama kubwa kutumia mitandao ya nchi jirani ya Kenya. Pia ameitaka TCRA kuyasimiamia kwa karibu kwa kuthibiti ubora wa baadhi ya makampuni ya simu yaliyopatiwa leseni ili wananchi wapate mawasiliano ya uhakika.
Mbunge Tadayo ametoa ushauri huo alipokuwa akichangia mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mei, 19,2021, katika Mkutano wa Tgatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jijini Dodoma.
Mdau nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Mbunge Tadayo akilipambania suala hilo....
Post a Comment