Taarifa iliyomnukuu Katibu Idara ya Bunge Baraza la Wawakilishi na Serikali za Mitaa, Hamad Yussuf, imesema mbunge huyo amefariki Dunia leo alfajiri akiwa katika Hospitali ya Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.
"Nasikitika kuwatangazia Kifo Cha Mhe Khatib Haji Mbunge wa Jimbo la Konde, ambaye umauti umemfika akiwa anapatiwa Matibabu katika hospitali ya Taifa Muhimbili Alfajiri ya leo, mipango ya mazishi inaendelea na tutajulishwa baadae kidogo.
Kwa Niaba ya Idara ya Bunge, Baraza la Wawakilishi na Serikali za Mitaa natoa pole kwa Kiongozi wa Chama na Viongozi wengine wote Familia, na Wananchi wa Jimbo la Konde, Allah Amsamehe makosa yake, ampe kauli thabiti ampe pepo ya Firdaus na sisi atujaalie mwisho mwema Aamin", amesema Hamadi Yussuf.
Kufuatia kifo hicho, huyu sasa ni Mbunge wa tatu kufariki Dunia katika Bunge la sasa la 12 lililoanza Novemba 2020, waliotangulia mbele za haki wakiwa ni aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Martha Umbulla, aliyefariki Januari 21, 2021, Mumbai nchini India alikokuwa akipatiwa na Atashasta Nditiye aliyefariki kwa ajali jijini Dodoma.
Post a Comment