Featured

    Featured Posts

MAJALIWA ATAKA HATUA ZAIDI ZICHUKULIWE KWA WANAOHUSIKA NA MFUMO WA LUKU

Dar es Salaam

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amemuagiza Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani asiishie kuwasimamisha kwa siku kumi tu meneja wa TEHAMA na wasaidizi wake, bali wakae pembeni hadi hapo uchunguzi zaidi utakapokamilika.

 

Ametoa agizo hilo leo Mei 20, 2021 alipozungumza na Menejementi na Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwenye makao makuu ya zamani Shirika hilo jijini Dar es Salaam.

 

“lazima tufundishane kuwa makini, kila siku lazima tukague vifaa vyetu ili huduma ipatikane muda wote. Hakuna kuwasimamisha kwa siku 10, wakae pembeni hadi timu inayochunguza itakapotoa matokeo.  Inawezekana sio wao tu, Waziri endelea na uchunguzi”

 

Aidha, Waziri Mkuu ameliagiza shirika hilo kuhakikisha wanakuwa na mfumo wa dharura ‘backup’ utakaotumika pindi kunapotokea changamoto za kimfumo

 

“Mmetengeneza usumbufu mkubwa sana, mlijua lazima kuwe na backup lakini hakuna, toka pale tulipoanza kutoa huduma mpaka leo kwanini hakuna backup, hilo ni jukumu lenu”.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi  na Menejimenti ya Shirika la Umeme Tanzania -  TANESCO kwenye Makao Makuu ya zamani ya Shirika hilo Ubungo jijini Dar es salaam, Mei 20, 2021.   Kushoto  ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana