Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita), Anthony Temu (kushoto) akiwaelekeza maofisa wa Halmashauri ya Manispaa ya Mufindi jinsi ya kujaza dodoso kwa kutumia mfumo wa Kobo wakati wa kikao cha maandalizi ya mafunzo kwa wanufaika wa Mkurabita wa Kijiji cha Lugodalutali yatakayofanyika Jumanne ijayo Juni Mosi, 2021.Kulia ni Afisa Kilimo, Mwamini Mwakyaka na Afisa Ushirika Pili Mwaipaja.
Afisa Maendeleo wa Halmashauri hiyo, Joha Kambala akielezea jinsi atakavyotoa mafunzo katika mafunzo hayo
Temu akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho cha maandalizi. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Na Richard Mwaikenda, Mufindi.
Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) umeandaa mafunzo ya kuwainua kiuchumi zaidi ya wanufaika 600 waliopatiwa Hati miliki za kimila za ardhi zao katika Kijiji cha Lugodalutali wilayani Mufindi, mkoani Iringa.
Akizungumza wakati wa kikao cha maandalizi kilichofanyika mjini Mafinga leo Mei 25, 2021, Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini wa Mkurabita, Anthony Temu amesema kuwa mafunzo hayo yatafanyika Jumanne ijayo Juni Mosi katika kijiji hicho ambapo yatakuwa mafunzo ya wazi kwa wananchi wote.
Amesema kuwa licha kuwafundisha jinsi ya kutumia hati miliki hizo kuwa dhamana ya kupatia mikopo benki na taasisi zingine za fedha, pia watapata mafunzo kutoka kwa watalaamu jinsi ya kuthamini mali zao, kanuni bora za kilimo, faida za kujiunga na Ushirika, jinsi ya kuweka kumbukumbu na kuchangamkia fursa mbalimbali ikiwemo mikopo ya halmashauri.
Katika mkutano huo watakuwepo watalaamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, maofisa wa Benki watakaoelezea kuhusu mikopo lakini pia wananchi wataruhusiwa kufungua akaunti za chap chap wakati mafunzo yakiendelea.
Vile vile atakuwepo mtaalamu wa masuala ya ufugaji wa nyuki kibiashara hasa kutokana na msaada wa mizinga 30 utakaotolewa na Mkurabita katika Kijiji hicho.
Post a Comment