Featured

    Featured Posts

MZEE PINDA, RC MAHENGE WAONGOZA UZINDUZI WA KAMPENI YA UPANDAJI MITI ZUZU, DODOMA

Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda akiongoza kupanda miti wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kupanda miti 10,000 katika Kata ya Zuzu, mkoni Dodoma leo Mei 15,2021.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa Mteule wa Singida, Dkt. Binilith Mahenge akiungana na Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti katika Kata ya Zuzu uliofanyika katika shule ya Sekondari ya Zuzu.
Paroko Pinoy Thomas wa Kanisa Katoliki Nzinje, Zuzu akipanda mti wakati wa kampeni hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Benki ya Exim, Stanley Kafu akishiriki kupanda miti wakati wa kampeni hiyo. Upandaji miti unaoratibiwa na Taasisi ya Habari Development (HDA) umefadhiliwa na benki hiyo.
Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Pinda, Mccelina Chuwa akipanda mti
Wadau mbalimbali wa mazingira wakipanda miti eneo la shule ya Sekondari Zuzu.


Wanafunzi wa shule ya Zuzu wakishiriki kupanda miti

Kikundi cha ngoma cha Mwino kikitumbuiza
Katibu wa Taasisi ya Habari Development, Bernard James akielezea umuhimu wa kupanda miti na kuifanya Dodoma ya kijani, lakini pia aliishukuru Benki ya Exim kufadhili kampeni hiyo ya upandaji miti.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Benki ya Exim, Stanley Kafu aakizungumza wakati wa kampeni hiyo na kuahidi kusaidia uchimbaji wa kisima cha maji ya kumwagilia miti hiyo pamoja na matumizi mengine ya binadamu.
Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti na kuwataka wananchi kushiriki kwa ukamilifu pamoja na kuitunza.


Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Mahenge akiwa na Waziri Mkuu mstaafu, Pinda


Wanafunzi wakibeba mbole ya kupandia miti

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge na Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda wakiwa na kikosi cha Taasisi ya Habari Development
 Imeandaliwa na Richard Mwaikenda Mhariri Blog ya Taifa ya CCM 0754264203
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana