Rais Samia Sulihu Hassan akizungumza, wakati wa mkutano wake na Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam, katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, leo.
Mlimani City, Dar es Salaam.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa onyo kwa watu wanaojihusisha na vitendo vya ujambazi na uhalifu katika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo amesema wanaofanya hivyo waache kupima kina cha maji.
Ametoa onyo hilo leo Mei 7, 2021 wakati anazungumza na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam ambapo ametumia nafasi hiyo kuzungmzia umuhimu wa kuendelea kulinda amani na usalama nchini.
"Tumeahidi kudumisha amani na usalama, kama wazee mlivyotuomba na hili tutasimia kwa nguvu zote.Leo nimesoma habari sio kwenye mitandao ya kijamii, wanajaribu kina cha maji, Dar naomba nitoe meseji wasijaribu kina cha maji, na katika mitandao ile kuna Kamanda ametajwa kuwa alikuwepo hapa Dar lakini ameondolewa.
"Mkuu wa Jeshi la Polisi uko hapa naomba hili ulifanyie kazi kuhusu huyo ambaye anatajwa kuwa alifanikiwa kudhibiti ujambazi.
Lakini turudi tena kwenye mila desturi zetu kwani hali ngumu za uchumi haifanyi mtu awe jambazi, hivyo turudi tena kwenye maadili ya watoto wetu.Tusimamie hili kwa nguvu zote," amesema Rais Samia.
Chanzo: Michuzi Blog
Post a Comment