Featured

    Featured Posts

WAZIRI NDALICHAKO AFUNGUA MAONESHO YA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU DODOMA+video

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt. Leonald Akwilapo (mbele) pamoja na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Omary Katanga wakitoka kukagua maabara inayohamishika  kwenye Maonesho ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu yaliyofunguliwa leo Mei 7,2021  na Waziri Ndalichako kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.


Waziri Ndalichako akipata maelezo kutoka kwa Clinton Joseph mbunifu wa mashine ya kutengeneza mifuko. Mashine hiyo ina uwezo wa kutengeneza mifuko 2000 kwa siku na mfuko mmoja huuzwa sh. 200.
Waziri Ndalichako akiangalia begi la shule linalotumia mionzi ya jua hivyo kumsaidia mwanafunzi kutumia mwanga kusomea maeneo yenye giza.
Wanafunzi wakionesha vigari na ndege za kuchezea walizozitengeza zinazotembea kwa kutumia mota.


Waziri Ndalichako akipata maelezo ya jinsi ya kustawisha nyasi za ngano kwa ajili ya malisho ya mifugo.
Waziri Ndalichako akipata maelezo ya gari lililobuniwa na mmoja wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo Morogoro (SUA) ambalo ni maalumu kwa ajili ya kumsaidia mkulima kurahisisha kazi zake. Gari hilo linauzwa sh. mil. 8.

Waziri Ndalichako akioneshwa kiti maalumu kwa ajili ya wagonjwa hospitalini.
Waziri akitembelea banda la Vodacom
Waziri Ndalichako akitembelea banda la Tigo.
Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt Akwilapo akizungumza maneno ya utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri Ndalichako kufungua rasmi maonesho hayo.
Sehemu ya washiriki wa maonesho hayo.
Waziri Ndalichako akihutubia wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

 

Mdau nakuomba uendelee kuona na kusikiliza Waziri Ndalichako na viongozi wengine wa wizara hiyo wakitembelea mabanda mbalimbali ya wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo... 

 

Mhariri Blog ya Taifa ya CCM

 0754264203
 

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana