Featured

    Featured Posts

RAIS SAMIA KWENDA KENYA KESHOKUTWA, KUZUNGUMZA NA RAIS KENYATTA NA KULIHUTUBIA BUNGE LA NCHINI HUMO

 

Ikulu, Chamwino.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan atafanya ziara rasmi ya siku 2 katika Jamhuri ya Kenya kuanzia krshokutwa Mei 5, 2021 kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Kenya,  Uhuru Kenyatta.


Taarifa iliyotolewa na Ikulu, Chamwino jijini Dodoma imesema, Rais Samia akiwa nchini humo, atafanya mazungumzo maalum na mwenyeji wake Rais Kenyatta na kisha atalihutubia Bunge la Kenya litakalojumuisha Wabunge wa Mabunge yote mawili ya nchi hiyo.


Taarifa hiyo imesema katika ziara hiyo Rais Samia atahudhuria na kuhutubia mkutano wa jukwaa la wafanyabiashara wa Kenya na Tanzania utakaofanyika Jijini Nairobi kwa lengo la kujadiliana masuala mbalimbali yahusuyo fursa za biashara na uwekezaji zilizopo Tanzania na Kenya.


Matukio ya ziara hii yatarushwa mbashara na vyombo vya habari vya redio, televisheni na mitandao ikiwemo youtube channel ya Ikulu Mawasiliano na akaunti rasmi za Instagram, Facebook na Twitter.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana