Mkuu mpya wa mkoa wa Dar es Salaam Komredi Amos Makalla amemaliza mgongano wa kiuongozi kati ya Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Spora Liana.
Utatuzi wa mgongano huo umefanyika leo katika kikao cha pamoja kilichoitishwa na Mkuu huyo mpya wa mkoa Dar es Salaam, na kuwakutanisha Meya Songoro na Mkurugenzi Spora Liana.
Mkuu wa mkoa amewataka viongozi hao kurejea ofisini na kufanya kazi kwa pamoja, kutekeleza miradi ya maendeleo na kutatua kero za wananchi.
Kwa upande wa Meya na Mkurugenzi wamemaliza tofauti zao na wameahadi kufanya kazi kwa pamoja kwa maslahi mapana ya wananchi.
Chini ni picha mbalimbali za tukio hilo👇
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Spora Liana wakishikana mikono mbele ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla (Katikati), leo.Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Spora Liana wakikumbaniana kwa furaha mbele ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, leo. Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla akuwa katika picha ya kumbukumbu na Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge (Kushoto) na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Spora Liana (Katikati) baada ya kikao, leo.
Post a Comment