Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo akivishwa skafu alipowasili Ofisi za CCM Mkoa wa Dodoma leo, tayari kuanza ziara ya kujitambulisha kwa wana CCM na wananchi Mei 21,2021.
Katibu Mkuu Chongolo na Naibu Katibu Mkuu, Christina Mndeme na baadhi ya timu ya sekretarieti yake wameanza ziara ya kujitambulisha kwa wanachama na wananchi ambapo leo ameanzia Mkoa wa Dodoma na Morogoro na kesho watakuwa Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam.
Waendesha bodaboda wakiongoza msafara wa Katibu Mkuu wa CCM ulipokuwa unaanza Makao Makuu ya CCM (Whitehouse) jijini Dodoma leo.
Katibu Mkuu, Chongolo akiwapungia mkono wananchi alipowasili Ofisi za CCM Mkoa wa Dodoma kujitambulisha na kuongea na wanachama.
Katibu Mkuu wa CCM, Chongolo na Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara, Mndeme wakitia saini kwenye kitabu cha wageni walipowasili Ofisi za CCM Mkoa wa Dodoma. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo, Godwin Mkanwa.
Post a Comment