KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Shaka Hamdu Shaka ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumaliza changamoto ya siku ya mbili ya umeme.
Shaka ametoa pongezi hizo leo jijini Dodoma wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM,Daniel Chongolo na wandishi wa habari.
Akizungumza wakati wa kumkaribisha Katibu Mkuu Chongolo, Shaka ametoa pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati kwa kumaliza changamoto hiyo.
" Ndugu Katibu Mkuu kabla sijakukaribisha niipongeze Serikali yetu chini ya Rais Samia kwa namna ilivyolishughulikia tatizo la ununuzi wa umeme kwa njia ya mtandao na kulimaliza na Sasa Kazi inaendelea.
Kupitia mkutano huu nitumie nafasi hii pia kuomba radhi kwa watanzania ambao wameiamini CCM kuiongoza, Ni matumaini yetu kwamba Serikali imefanyia kazi changamoto hiyo na haitojirudia," Amesema Shaka.
Post a Comment