Na Shabani Rapwi, Dar es Salaam
Klabu ya Simba SC ya Tanzania imepokea kichapo cha mabao 4-0 dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ulipigwa kwenye uwanja wa FNB, Johannesburg. 

Mabao ya Kaizer Chiefs katika mchezo huo yamefungwa na Eric Mathobo dakika ya  6', Samir Nurkovic aliyefunga mabao mawili dakika ya 34' na dakika ya 57' pamoja na Leonardo Castro dakika ya 63'.

Mchezo wa robo fainali ya pili itapigwa Mei 22, 2021 katika uwanja wa Benjamin Mkapa