Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Usalama wa Chakula Wizara ya Kilimo, Josephine Amollo akihutubia wakati wa ufunguzi wa Semina ya Waandishi wa Habari juu ya Uchafuzi wa Sumukuvu na Athari zake katika Usalama wa Chakula, Afya na Uchumi jijini Dodoma leo Mei 18,2021.
Mratibu wa Mradi wa Mdhibiti Sumukuvu (TANPAC), Clepin Josephat akielezea umuhimu wa semina hiyo kwa waandishi wa habari na jamii kwa jumla wakati wa ufunguzi wa semina hiyo.
Rais wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma (CPC), Yusuf Mussa akitoa shukrani baada ya ufunguzi kufanywa na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Usalama wa Chakula, Josephin Amollo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara hiyo.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Kilimo, Revocatus Kassimba akitoa neno la utangulizi kabla ya Mgeni rasmi kufungua semina hiyo ya siku mbili na kuelezea lengo ikiwemo wanahabari kuijua vilivyo sumukuvu na kutoa taarifa sahihi kwa jamii.
Na Richard Mwaikenda, Dodoma
Waandishi wa habari kutoka mikoa tisa wamepigwa msasa kuhusu Sumukuvu katika semina iliyoandaliwa na Wizara ya Kilimo jijini Dodoma.
Semina hiyo ya siku mbili iliyowakutanisha waandishi wa habari kutoka mikoa tisa nchini moja ya malengo yake ni kuelimisha jamii juu ya Sumukuvu njia mbalimbali za kufikisha ujumbe zikiwemo utumia vyombo vya habari ni muhimu ili kuhakikisha jamii inatambua tatizo la sumukuvu na namna ya kudhuibiti madhara yake.
Akizungumza neno l utangulizi kabla ya ufunguzi, Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano wa wizara hiyo, Revocatus Kassima, alisema kuwa wamendaa semina hiyo ili wanahabari waielewe sumukuvu na kuweza kutoa taarifa sahihi juu ya sumukuvu kwa jamii na katika namna ambayo haitaleta taharuki kwa umma.
Mafunzo hayo yameandaliwa kwa waandishi wa habari wa redio, televisheni, magazeti, majarida na mitandao ya kijamii kutoka mikoa tisa nchini.
Akizungumza leo Mei 18,2021 jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na chakula Josephine Amollo amesema Wizara ya kilimo iliandaa mradi ambao ulizinduliwa mwaka 2019 na kuanza kufanya kazi 2020.
Amesema mradi wa Sumukuvu ulitambuliwa baada ya kugundua madhara kwa wananchi yamekithiri ambapo serikali ikazindua mradi wa kudhibiti uchafuzi wa Sumukuvu katika Usalama wa chakula.
Amollo, amesema kuwa Sumukuvu inaleta hofu katika jamii hivyo wanahabari wanayakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuielimisha jamii juu ya Sumukuvu na kuondoa taharuki katika jamii kwani sumukuvu ilikuwepo tangu hapo zamani.
Mwanaidi Kiya kutoka Wizara ya kilimo Kitengo Cha Usalama na Uhakika wa Chakula amesema Takwimu kutoka Shirika la Chakula Duniani zinasema kwamba mtu mmoja Kati ya Watu 10 wanakufa kila mwaka kutokana uchafuzi wa chakula.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video yaliyojiri kwenye semina hiyo.....
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203
Post a Comment