Featured

    Featured Posts

CHONGOLO AWATAKA WABUNGE KUTUA MIZIGO YAO KWA KUSIMAMIA VIZURI ASILIMIA 4 ZA MIKOPO KWA WANAWAKE+video

 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo akihutubia wakati wa ufunguzi wa Baraza Kuu la Wanawake la Umoja wa Wanawake wa CCM kwenye Ukumbi wa NEC (White House), Makao Makuu ya chama hicho jijini Dodoma leo, ambapo pamoja na mambo mengine  amewataka wabunge waliopitia UWT kutoa taarifa  kila mwaka za ni jinsi gani wamewapambania wanawake katika mikoa yao ikiwemo matumizi ya asiliamia 4 za wanawake zinazotengwa katika Halmashauri.

Amewataka wabunge hao kuitua mizigo mizito ya kutoa fedha zao kuwasaidia wanawake bali wajikite  kusimamia mgao huo wa asilimia 4 kwa wanawake kwa kupanga mipango ya kuwaendeleza na kujua zimetumikaje. 

Pia, Baraza  hilo linapaswa kujua Nchi nzima fedha kiasi gani zimetengwa, zimetolewa kwa kina mama wangapi kwani anazotaarifa  kuna baadhi ya viongozi wamekuwa wakijinufaisha binafsi na fedha hizo.

Katibu Mkuu wa CCM, Chongolo akisisitiza jambo.

Baadhi ya wabunge wa Vit Maalumu wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Chongolo na viongozi wa UWT..


Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Taifa ,Gaudensia Kabaka,akizungumza katika Mkutano wa  Baraza Kuu la UWT Taifa,uliofanyika leo Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa UWT, Queen Mlozi akisema maneno ya utangulizi wakati wa  ufunguzi wa mkutano  wa Baraza Kuu.

Sehemu ya wajumbe wa Baraza hilo.

Sehemu ya wajumbe wa baraza hilo wakiwa katika mkutano akisikiliza kwa makini wakati Katibu Mkuu Chongolo akihutubia

PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

Mdau nakuomba uendelee kusikiliza clip hii ya video ujue Katibu Mkuu Chongolo alichozungumza kwenye mkutano huo.....


author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana