Featured

    Featured Posts

DC MPOGOLO ATOA MADAFTARI YA SH. MILIONI 10 KWA WANAFUNZI WANAOJIANDAA NA MITIHANI DARASA LA NNE NA LA SABA, WILANI IKUNGI

Na Dotto Mwaibale, Ikungi
MKUU wa Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida, Edward Mpogolo ametoa madaftari yenye thamani ya Sh. milioni 10 kwa wanafunzi wa shule za msingi wilayani humo ikiwa ni kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika.

Akizungumza leo wakati akikabidhi madaftari hayo Mpogolo alisema msaada huo umelenga kuwasaidia wanafunzi wa darasa la nne na la saba ambao wanaendelea na masomo kwa ajili kujiandaa na mitihani yao ya mwisho.

"Msaada huu nilioutoa umelenga kuwasaidia wanafunzi hawa ili waweze kujiandaa vema na mitihani yao ambayo wataifanya mwaka huu," alisema Mpogolo.

Mpogolo alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wadau wote wa maendeleo waliofanikisha kupatikana kwa msaada huo.

Afisa Elimu Vifaa na Takwimu wa wilaya hiyo, Imani Maketa, alisema msaada huo utawaongezea mori wa kufanya vizuri mitihani yao wanafunzi hao. 

Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Ikungi Mchanganyiko, Asia Hassani akizungumza kwa 

niaba ya wenzake alimshukuru Mpogolo kwa kuwapa msaada huo ambao umetolewa kwa wakati na kuwataka wadau wengine kuiaga mfano huo.

Wanafunzi waliopata msaada huo ni kutoka shule ya msingi 15 wilayani humo ambazo  ni Ikungi Mchanganyiko, Dung'unyi, Siuyu, Msungua, Minyinga, Mandimu, Mkenene, Choda na Kaugeri (Mdunghuyu).

Habari katika Picha👇
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Edward Mpogolo, akiwapatia madaftari Wanafunzi wa Shule ya Msingi Choda alipotoa msaada wa madaftari ya sh. Milioni 10 kwa wanafunzi wanaojiandaa na mitihani ya darasa la nne na la saba katika wilaya hiyo, katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, jana.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida, Edward Mpogolo, akiwapatia madaftari Wanafunzi wa Shule ya Msngi Ikungi Mchanganyiko ikiwa ni kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika.

Wanafunzi wa Shule ya Msngi Ikungi Mchanganyiko wakishangilia kuonesha furaha zao baada ya kupatiwa msaada huo.

Furaha za wanafunzi  baada ya kupatiwa msaada huo.

Diwani wa Kata ya Choda, Steven Mtyana (kulia), akiwapatia madaftari Wanafunzi wa Shule ya Msingi Choda yaliyotolewa na Mpogolo

Mwenyekiti wa Kijiji cha Choda,  Charles Elias, akiwapatia madaftari Wanafunzi wa Shule ya Msingi Choda yaliyotolewa na Mpogolo.
Mwalimu Mkuu wa  Shule ya Msingi Choda, Hilda  Paul, akiyangalia madaftati hayo kabla ya kuwapatia wanafunzi.
Afisa Elimu Vifaa na Takwimu wa wilaya hiyo, Imani Maketa, akiwapatia madaftari Wanafunzi wa Shule ya Msingi Choda yaliyotolewa na Mpogolo.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Choda, Eliufoo Mwanja, akiwapatia madaftari WanafunziA wa Shule ya Msingi Choda yaliyotolewa na Mpogolo.
Afisa Tarafa wa Ikungi, Josephina  Kadaso, akiwapatia madaftari WanafunziA wa Shule ya Msingi Choda yaliyotolewa na Mpogolo.
Mwenyekiti wa  Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Choda, Iddi Kiteu, akiwapatia madaftari Wanafunzi wa Shule ya Msingi Choda yaliyotolewa na Mpogolo

DC Mpogolo, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Kijiji cha Choda.

Sehemu ya madaftari yaliyotolewa kwa wanafunzi wilayani humo.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana