Featured

    Featured Posts

IGP SIRRO APANGUA MAKAMANDA WA WATATU WA MIKOA, LEO

 

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Simon Sirro (pichani) leo Juni 4,2021 amefanya mabadiliko ya Makamanda watatu wa Polisi wa mikoa ya Ilala, Shinyanga na Songwe.

Katika mabadiliko hayo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) ACP Debora Magiligimba aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga amehamishiwa Mkoa wa Kipolisi Ilala Kanda Maalumu ya Dar es salaam,akichukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Janeth Magomi anayeenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe.

Katika Mabadiliko hayo, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), George Kyando aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga :chanzo Dira makini 
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana