Featured

    Featured Posts

URASIMISHAJI ARDHI UNAOFANYWA NA MKURABITA UNAPUNGUZA MIGOGORO-DED KILOSA+video


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, Asajile Mwambando (kuahoto) akizungumza na Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita), Anthony Temu (kulia) wakati timu ya Mkurabita ilipokwenda kujitambulisha kwa ajili kuanza kazi ya urasimishaji wa ardhi ya wakulima wadogo  100 wa zao la miwa katika Kijiji cha Mkundi, Kata ya Dumila kwa lengo la kuwapatia hati miliki za kimila zitakazotumika kuweka dhamana kukopa fedha benki za kuboresha miradi yao ikiwemo zao la miwa.

Mkurugenzi Mtendaji Mwambando aliomba Mkurabita isiishie kurasimisha kwenye kijiji hicho kimoja, bali ikiwezekana wafanye kazi hiyo kwa upana zaidi hata katika vijiji vingine wilayani humo, akidai urasimishaji huo unasaidia kupunguza migogoro ya ardhi na kuleta utulivu.

Mkurabita kwa kushirikiana na maafisa wa Halmashauri, watendaji kata na viongozi wa vijiji na vitongoji wameanza kazi ya upimaji ardhi za mashamba leo Juni 4,2021 katika Kijiji hicho chenye vitongoji vitatu ambavyo ni;Kichangani, Visalaka na Matale.

Kabla ya kuanza uongozi wa Mkurabita ukiongozwa naTemu ulifanya jana kikao cha kuweka mambo sawa na Halmashauri ya Kijiji cha Mkundi pamoja na mkutano wa hadhara wa wananchi wa kijiji hicho ambapo waliazimia kwa kauli moja kuanza urasimishaji wa mashamba yao.

Mwambando (wa pili kulia) akimtambulisha Anthony Temu (kushoto) kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Adam Mgoyi (wa pili kushoto). Kulia ni Afisa Ardhi wa Wilaya, Cheyo Nkelege. 

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza/kuona kupitia clip hii ya video Mkurugenzi Mtendaji wa Kilosa, Mwambando akizungumza maneno hayo mbele ya Meneja wa Mkurabita, Temu......

Imeandaliwa na Richard Mwaikenda

Mhariri Blog ya Taifa ya CCM

0754264203


 
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana