Featured

    Featured Posts

JAFFAR HANIU ACHUKUA MIKOBA YA GERSON MSIGWA, IKULU


Jaffar Haniu na Gerson Msigwa


Ikulu, Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa vyombo vya habari vya Africa Media Group Limited Jaffar Mohamed Haniu kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.


Taarifa iliuotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu ambaye anaondoka Gerson Msigwa, imesema, Haniu anachukua nafasi ya yeye (Msigwa) ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali.


"Uteuzi wa Bw. Haniu umeanza leo Juni 09, 2021", taarifa hiyo imesema.


Wakati huohuo, mbali na taarifa hiyo ya Ikulu, Msigwa ameshukuru sana kwa ushirikiano aliopewa wakati akiwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.


"Aidha naomba kuchukua nafasi hii kuwashukuru sana kwa ushirikiano mkubwa mlionipa wakati wote nikiwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.


Nilikuwa na wakati mzuri sana wa kushirikiana nanyi na kwa pamoja tumefanya mambo mengi katika safari ya kuleta mageuzi ya habari na mawasiliano katika Kurugenzi hii.


Kama kuna mahali tulikwazana naomba tusameheane. Lakini nataka kuwahakikishia kuwa kama ilitokea hivyo ni kwa sababu ya kutekeleza majukumu tu na sio vinginevyo.


Kwa sasa nipo Idara ya Habari Maelezo, najua tutakuwa na wakati mzuri zaidi wa kushirikiana kwa sababu huko ndio nakwenda kutekeleza majukumu yatakayoniweka karibu nanyi zaidi. 


Nawaahidi ushirikiano, upendo na mshikamano mkubwa. Aidha, nawatakia kila la kheri katika majukumu yenu. Mungu awabariki sana", ameandika Msigwa.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana