CCM Blog, Dodoma, leo.
Kikao cha Kamati Kuu (CC) ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimefanyika leo jijini Dodoma, kikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan.
Kikao hicho ambacho ni cha kawaida na cha kwanza kwa Mwenyekiti mpya wa CCM, Rais Samia na Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo, kimefanyika kujadili masuala mbalimbali ya Chama.
Kikao hicho kimefanyika baada ya Kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kilichofanyika jana Juni 21, chini ya Mwenyekiti wake, Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo.
Picha👇
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi, akioitia nakabrasha, kabla ya kuanza Kikao cha Kamati Kuu (CC) ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kilichofanyika leo Jumanne Juni 22, 2021 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre, Jijini Dodoma. Kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka akimwelekeza jambo Katibu wa NEC Oganaizesheni Moudline Castico kabla ya kuanza kikao hicho.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEixYY9QqOkabU-iD0BvSG0zdq9HnTHqPv59h2aw9l0L2jgPBi-iPxVlO_ZUekSYrF79HNHNx_sRnODSpU7k_OxXUJAdy8_zrQA64s5cl-rnUoyqx1I8IaizjgF-FdRoYISlc-UebqEnTtQ/w400-h227/IMG_20210622_145156.jpg)
Post a Comment