Featured

    Featured Posts

RAIS SAMIA AKERWA NA KASI NDOGO UJENZI WA MRADI WA MWENDO KASI MBAGALA, AMTAKA MKANDARASI KUONGEZA KASI

Ikulu, Dar es Salaam, leo

Rais Samia Suluhu Hassan amekerwa na kasi ndogo ya ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo araka (BRT) awamu ya pili katika maeneo ya Mbagala Bendera Tatu na Mbagala Zakhem ambako ameshuhudia kuwa  ujenzi umefikia asilimia 16 tu badala ya asilimia 60 iliyotarajiwa.


Kufuatia hali, amemtaka mkandarasi wa mradi huo kuongeza kasi na kuacha visingizio ili mradi ukamilike na kukidhi matarajio na malengo ya serikali kuboresha hali ya usafiri kwa wananchi.


Amewahakikishia wananchi kuwa mradi huo pamoja na miradi mingine inayotekelezwa na Serikali katika maeneo mbalimbali nchini itakamilishwa kama ilivyopangwa na pale ambapo mkandarasi atachelewesha hatua zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria.


Rais Samia pia amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala Wilayani Kinondoni ambapo pamoja na kupokea maelezo ya Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dk. Zavery Benela amewatembelea wagonjwa wanaopatiwa matibabu ya nje na waliolazwa wodini.


Katika ziara hiyo, Rais Samia ametoa msaada wa shuka 200 kwa ajili ya wagonjwa katika hospitali hiyo na amewahakikishia wananchi kuwa Serikali itachukua hatua zaidi kutatua tatizo la upatikanaji wa dawa, kuboresha maslahi ya Madaktari na Wauguzi na kuboresha mazingira ya hospitali hiyo.


Aidha, Rais Samia amewataka Watanzania wote kuendelea kuchukua tahadhari zinazoshauriwa na wataalamu kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Korona (Covid-19).


Katika Soko Kuu la Kariakoo, Mhe. Rais Samia amewatembelea wafanyabiashara wanaouza bidhaa zao hasa vyakula ndani ya soko kuu na kujionea msongamano mkubwa wa bidhaa, wafanyabiashara na wananchi wanaokwenda kununua bidhaa.


Wafanyabiashara hao wamelalamikia tatizo la ugumu wa uingizaji wa bidhaa kutokana na njia za kuingia sokoni kufungwa na wafanyabiashara wengine ambao wamepanga bidhaa zao njiani, tozo kubwa za vizimba,  ushuru wa bidhaa zinazoingia sokoni na gharama za usafishaji wa bidhaa kutokana masoko mengine.


Baada ya kujionea hali halisi, Mhe. Rais Samia ameelezea kusikitishwa kwake na hali hiyo na amesema Serikali itafanya tathmini ya uendeshaji wa soko hilo ili kurekebisha dosari zilizopo ikiwemo kuratibu uingizaji wa mizigo, mpangilio wa bidhaa sokoni na kuboresha usafi.


Ameagiza kusimamishwa mara moja kwa uongozi wa Shirika la Masoko Kariakoo ili kupisha uchunguzi kufuatia malalamiko mbalimbali yaliyotolewa na wafanyabiashara dhidi ya viongozi hao, lakini wakati hatua hizo zinachukuliwa amewataka wafanyabiashara kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia taratibu na sheria.


Katika soko la Kisutu, Rais Samia amejionea kazi za ukamilishaji wa soko hilo ambalo linatarajiwa kukamilika wiki ijayo na kuwarejesha wafanyabiashara waliokuwa wameondolewa kupisha ujenzi wake.

Rais Samia Suluhu Hassan akimpa pole mmoja wa wagonjwa katika Hosoitali ya Mwananyamala, leo.
Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi katika Hospitali ya Mwananyamala, leo.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana