Na Lydia Lugakila,Bukoba
Wakuu wa wilaya za Karagwe Bihalamuro na Misenyi walioapishwa Mkoani Kagera wametakiwa kusimamia nidhamu katika wilaya zao ikiwemo kujiepusha na masuala ya ubinafsi na upendeleo.
Wakuu wa wilaya za Karagwe Bihalamuro na Misenyi walioapishwa Mkoani Kagera wametakiwa kusimamia nidhamu katika wilaya zao ikiwemo kujiepusha na masuala ya ubinafsi na upendeleo.
Akizunguza baada ya kuwaapisha wakuu wa wilaya hizo mkuu wa mkoa wa Kagera meja Jenerali Charles Mbuge amesema kuwa viongozi hao wanapaswa kuwajibika ipasavyo na kufanya kazi kwa weledi ikiwa ni pamoja na nidhamu katika maeneo yao ya kazi kwani kupata nafasi hiyo ni heshima kubwa kwao.
"Msiwe masikio yanayozidi kichwa wekeni nidhamu ya kazi fanya kazi bila ubaguzi wa aina yoyote tatueni migogoro ya wananchi" alisema meja Jenerali Mbuge.
Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa hategemei kuona kiongozi yeyote kwa upande wa watendaji wa sekta za umma na zisizo za umma kuwa wabinafsi na kubaguana badala yake washirikiane katika kujenga mkoa huo.
Kwa upande wa mkuu wa wilaya ya Bukoba Moses Machali amezihimiza taasisi zote pamoja na wananchi kushirikiana katika shughuli za maendeleo na kuwataka wakuu wa wilaya wapya kutumia nyenzo zao walizokabidhiwa kuzipitia ili kujua kanuni na taratibu katika majukumu yao.
Hata hivyo katibu tawala Mkoa wa Kagera Profesa Faustin Kamuzora amewapongeza viongozi hao na kuwasisitiza kutumia muda wao kusikiliza migogoro ya wananchi kushauri na kuitatua.
Post a Comment