Featured

    Featured Posts

RC KUNENGE AZINDUA MAGARI YA HONGYANG KATIKA KIWANDA CHA GF, AKEMEA WATENDAJI WANAOWATIA HOFU WAWEKEZAJI

Kibaha, Pwani

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amezindua awamu ya  pili ya utengenezaji wa magari aina ya Hongyang katika Kiwanda cha magari cha GF Assemblers cha Kibaha mkoni Pwani.


Akizungumza baada ya uzinduzi wa magari hayo leo Kiwandani hapo, Kibaha mkoani Pwani, RC Kunenge amekemea baadhi ya tabia za Watendaji wa Serikali za kupishana katika ofisi za wawekezaji kwa visingizio mbali mbali.


Kunenge amevitaja baadhi ya visingizio baadhi ya Watendaji ha wa Serikali kuwa ni pamoja na kulazimisha kuonana na wamiliki au kuzingizia kutaka kufanya ukaguzi  hali inayowafanya wawekezaji kuwa na hofu na hivyo kushindwa kutimiza majukumu yao vizuri.


Kunenge amesema Serikali ya mkoa wa Pwani chini yake inahakikisha inapata maendeleo kwa kuongeza fursa ya biashara na uwekezaji wenye mazingira rafiki na utawala bora kwa hivyo hataki kusikia au kuona watendaji wanakua kikwazo katika kufanikisha mpango huo na kwamba hatawavumilia.


"Wakati Serikali ikijenga mazingira rafiki na wawekezaji sisi wenyewe maafisa wa Serikali tumekuwa kikwazo, hii haikubaliki", amesema Kunenge.


Nae Meneja wa kampuni  GF Vehicle Assemblers , Ezra Mereng amesema lengo Kampuni hiyo ni kuunda kila aina ya chapa (brand ) ya magari kwa kuwa teknolojia na mitambo waliyonayo inauwezo wa kuunganisha magari aina zote kwa viwango na vigezo vya Kitaifa na kimataifa. 


Mereng amesema kiwanda hicho kilianza kwa kuunda magari chapa ya FAW na sasa  wamezindua  chapa nyingine  ya Hongyang na kuwataka wadau na Kampuni zingine  za magari kuacha kuagiza nje ya nchi badala yake wapeleke GFA kuundiwa (Assembling) kwa kuzingatia vigezo vyote vya kimataifa.


Habari Picha👇

Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge (katikati), akikata utepe kuzindua awamu ya pili ya utengenezaji wa gari mpya la kubebea mizigo la anina ya Hongyang katika kiwanda cha GF kilichopo Kibaha mko wa Pwani, leo.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha GF Assemblers, Imrani Karmali,  baada ya  uzinduzi wa awamu ya pili ya utengenezaji wa gari mpya la kubebea mizigo la anina ya Hongyang katika Kiwanda hicho Kibaha mkoni Pwani leo.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge,  akipokea zawadi maalum kutoka kwa Mkurugezi wa Kampuni ya GF Assemblers Imrani Karmali, wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya utengenezaji wa gari jipya la kubebea mizigo la anina ya Hongyang katika kiwanda hicho Kibaha mkoni Pwani, leo. 
Jopo la Wataalam Watanzania na Wachina walioshiriki kutengeneza gari mpya la kubebea mizigo la aina ya Hongyang katika kiwanda cha GF kilichopo Kibaha mko wa Pwani wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi huo, leo. (Picha zote na Mpigapicha Maalum) Mpigapicha Maalum)
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana