Featured

    Featured Posts

ZIARA MWENYEKITI CCM WILAYA KIBAHA MJINI, KAMATI YA SIASA KATA KONGOWE

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya Ya Kibaha Mjini, ndugu Maulid Bundala ameendelea na ziara zake katika wilaya hiyo, safari hii akitembelea Kata Kongowe, azma kubwa ikiwa ni kukumbushana kuimarisha chama na kujibu kero za wananchi.
Pamoja na mambo mengine, katika ziara hiyo ya Kongowe aliyoambatana na wajumbe wa kamati ya siasa wilaya, ndugu Bundala aliwataka viongozi wa ngazi zote wa CCM kuhakikisha wanashirikiana na viongozi wa Serikali na wananchi kwa ujumla kutatua kero za wananchi, kuzingatia utekelezaji wa Ilani ya CCM, kusimamia kwa ufasaha katiba na kanuni za chama.
Wiki iliyopita mwenyekiti huyo na kamati ya siasa walifanya ziara Mtaa wa Vikawe Shule, Kata ya Pangani ambako pamoja na mambo mengine aliagiza Takukuru kuchunguza mgogoro wa ardhi unaodaiwa kuwahusisha viongozi wa Serikali.
Kata ya Pangani inatajwa kuwa kinara wa vitendo vya utapeli wa ardhi katika wilaya ya Kibaha hali inayosababisha migogoro isiyoisha. Baadhi ya viongozi wanatajwa kuhusika moja kwa moja kutapeli ardhi ya wananchi na ile ya Serikali (Mitamba), huku baadhi yao wakidaiwa kukesha kwa waganga na kuendekeza vitendo vya rushwa ili waweze kuendelea kuwa huru na utapeli.
Licha ya baadhi ya viongozi wa Serikali kushtakiwa na wananchi katika mabaraza ya ardhi na mahakamani, hakuna aliyewahi kuhukumiwa faini au kifungo. Wananchi wanaamini Mkurugenzi wa TAKUKURU Taifa ana kila sababu za kutupia jicho kinachoendelea Pangani ili kukomesha utapeli wa ardhi unaosimamiwa na baadhi ya viongozi ikiwamo kuendelea kuuza ardhi ya Serikali (Mitamba) na kujipatia mamilioni ya fedha huku wakiwashawishi wananchi waliowauzia waseme hawajauziwa bali wamevamia.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana