Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 22 Juni, 2021 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya wawili (2) kama ifuatavyo:-
Amemteua Bw. Suleiman Yusuph Mwenda (pichani) kuwa Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida. Mwenda anachukua nafasi ya Bw. Kenan Laban Kihongosi ambaye amepangiwa majukumu mengine.
Kabla ya uteuzi huo, Mwenda alikuwa Katibu Msaidizi Idara ya Oganaizesheni ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Makao Makuu Jijini Dodoma.
Aidha, Mhe. Rais Samia amemteua Bw. Lupakisyo Andrea Kapange kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu. Bw. Kapange anachukua nafasi ya Dkt. Charles Mhina ambaye atapangiwa majukumu mengine.
Kabla ya uteuzi huo, Kapange alikuwa Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Tanga.
Uteuzi huo umeanza leo tarehe 22 Juni, 2021.
Jaffar Haniu
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.
Post a Comment