Featured

    Featured Posts

DKT. GWAJIMA AKUTANA NA UONGOZI WA MOI

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na Watoto Mh Dkt Dorothy Gwajima akizungumza na uongozi pamoja na watumishi wa MOI leo katika ukumbi wa jengo jipya la MOI. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA).

17/7/2021.Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima  leo amekutana na kufanya kikao na Uongozi wa Taasisi ya Tiba na Mifupa (MOI).

Dkt. Gwajima ameipongeza Taasisi ya Mifupa MOI kwa kendelea kutoa huduma bora kwa Watanzania kwa kipindi cha miaka 25.


“ Hongereni mnafanya kazi nzuri, nimekuja hapa tujadiliane ili tuone ni namna gani MOI itafikisha miaka 30 ikiwa bora Zaidi, kueni huru kuchangia mada ili tusonge mbele Zaidi.”  Alisema Dkt Gwajima


Amesema pamoja na huduma nzuri nafahamu kwamba Kuna changamoto nyingi ambazo zinahitaji kutatuliwa ili tuendelee kutoa huduma 

Pamoja na mambo mengine.


Dkt. Gwajima amepokea maoni, michango pamoja na changamoto mbalimbali zinazolenga kuboresha hali ya utoaji huduma katika Taasisi yaTiba na Mifupa (MOI).


Hata hivyo Dkt.Gwajima amewapa siku kumi Taasisi hiyo kuandaa taarifa watashughulikiaje changamoto zilizo ndani ya uwezo na kuziwasilisha kwake.


Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini MOI Prof. Charles Mkonyi amesema Taasisi ya Tiba na Mifupa (MOI) ina mpango wa kuanzisha kliniki katika wilaya za mkoa wa DSM ili kuwasogezea huduma Wananchi.


“Pamoja na kuanzisha hizi kliniki pia tunalenga kujenga hospitali ya kisasa ya utengamao katika kiwanja cha MOI kilichopo Mbweni Mpiji jiji Dar es. Salaam,  Alisema Prof. Mkonyi.


Mkurugenzi mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface amesema Taasisi ya MOI imeendelea kusogeza huduma kwa wananchi ili kupunguzia adha ya kusafiri kufuata huduma Dar es Salaam.


“Tumesogeza huduma za kibingwa za ubongo KCMC pamoja na Bugando tumesogeza huduma za Mifupa, Hospiali ya kanda Mbeya na Nyangao Lindi Alisema Dkt. Boniface.


Dkt. Boniface amesema Maabara ya kisasa ya Ubongo (Angio Suit) iliyoanzishwa hivi karibuni tayari wagonjwa 27 wameshafanyiwa upasuaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akitoa taarifa ya utendaji wa MOI.

Prof. Charles Mkony akimkaribisha Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na watoto azungumze na Uongozi wa MOI leo katika ukumbi wa jengo jipya la MOI.


Baadhi ya Wakuu wa vitengo wakimsikiliza Waziri Gwajima alipokuwa akizungumz na Uongozi mzima wa Taasisi hiyo




Mkurugenzi Rasilimali watu na Utawala Steria Sanga (aliye simama) akifafanua jambo mara alipoulizwa swali na Waziri  
  MenejaUstawi wa Jamii na Uhusiano wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI). Almasi Jumaa akifafanua jambo mara baada ya kuulizwa swali na Waziri Gwajima 


 Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la MOI Privatus Masula (kushoto) akiwa na wenzake wakimsikiliza kwa umakini Waziri. Dorothy Gwajima mara alipokutana na uongozi pamoja na watumishi wa MOI leo katika ukumbi wa jengo jipya la MOI.






author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana