Wananchi wa kijiji cha Lufumbu wakimshangilia mbunge wao Joseph Kamonga baada ya kuwasili katika eneo la mkutano hapo jana.
======
Changamoto ya maji safi na salama imekuwa ni tatizo kubwa kwa maeneo mengi ya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe na kupelekea wananchi kutumia maji ya mito ikiwemo na kutembea kwa umbali mrefu katika kuyafuata maji hayo.
Kutokana na changamoto hiyo mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga amepambana katika kuhimiza serikali ili iweze kuleta miradi ya maji katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo ikiwemo kata ya Mlangali ambapo juhudi hizo zimezaa matunda kwani tayari baadhi ya maeneo yamefanikiwa kupata fedha za kuanzishwa kwa miradi hiyo.
Akizungumza katika mkutano wa wananchi katika kijiji cha Lufumbu kata ya Mlangali pamoja na kijiji cha Ligumbilo wilayani humo Mbunge huyo amesema kuwa tayari serikali kupitia Wizara ya Maji- Tanzania] imesha wasilisha kiasi cha shilingi milioni 50 kwaajili ya ujenzi wa mradi wa maji katika kata ya Mlangali huku kijiji cha Liughai kilichopo kata ya Masasi kikitengewa milioni 381 na kijiji cha Kiyogo milioni 268 pamoja na maeneo mengineyo.
Post a Comment