Featured

    Featured Posts

PROFESA KAMUZORA AZINDUA RASMI CHANJO YA KORONA MKOANI KAGERA, LEO

Na Lydia Lugakila, Bukoba

Katibu Tawala mkoa wa Kagera Prof. Faustin Kamuzora amezindua chanjo dhidi ya UVIKO- 19 na kuwataka wananchi Mkoani humo kujitokeza kwa wingi kupata chanjo hiyo na kuwapuuza wanaopotosha juu ya chanjo hiyo.


Amezindua chanjo hiyo leo Agosti 4, 2021 katika ukumbi wa hospitali ya Rufani ya mkoa huo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Kagera meja Jenerali Charles Mbuge.


Akizindua chanjo hiyo katibu tawala huyo amesemshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suruhu Hassan kwa kukubali kupokea chanjo hiyo  kwa ajili ya afya za watanzania huku akiwaomba wananchi mkoani humo na watanzania kwa ujumla kujitokeza kuchanjwa.


"Chanjo hii sio lazima ni hiari  niwaombe wananchi jitokeze mkachanjwe msiogope ni chanjo ya kawaida imefanyiwa majaribio na kupitishwa na shirika la afya duniani waliochanjwa wako salama wapuuzeni wanaopotosha  ",amesema Kamuzora.


Akikumbushia katika historia kwa mwaka 1918-1920 katibu tawala huyo amesema kuwa gonjwa kama hilo liitwalo mafua ya Kiispanish lilitikisa na watu waliopinga chanjo yake waliotoa taarifa za upotoshaji ndio waliougua na kupata madhara zaidi, huku akiwahimiza watumishi wa afya, wenye magonjwa sugu wenye zaidi ya miaka 50 kujitokeza kupata chanjo hiyo.


Katika hatua nyingine katibu tawala  amewasisitiza wananchi kubadili tamaduni kwa kwenda na wakati hasa kubadili ratiba za misiba kwa kutokaa muda mrefu msibani Kama ilivyokuwa kwa kipindi cha nyuma kwani mikusanyiko Kama hiyo ndiyo hatari zaidi.


Aidha mganga mkuu wa mkoa huo Dr Issasenda Kaniki amesema mapambano dhidi ya Covid- 19 mkoa huo umefanikiwa kufuata kanuni zote za afya na pia  dozi za kutosha zimapatikana ambapo halmashauri 8 na vituo 18 tayari wanazo chanjo hizo.


Naye mratibu wa chanjo mkoa wa Kagera Zablon Segeru amesema kuwa chanjo hiyo itatolewa katika hospitali ya rufaa ya mkoa huo na kituo cha afya Zam zam.

Katibu Tawala mkoa wa Kagera Prof. Faustin Kamuzora akipata chanjo cha Uviko 19, baada ya kuizindua rasmi leo katika ukumbi wa hospitali ya Rufani ya mkoa.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana