Kaimu Mkurugenzi wa Kurasimisha Ardhi na Biashara wa Mpango wa Kurasimisha Ardhi na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Jane Lyimo akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha wadau wakati wa kuwasilisha Taarifa ya Tathmini ya Utafiti wa Msingi wa Biashara ya Bodaboda/Bajaji katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma kilichofanyika Ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu jijini Dodoma leo Agosti 11,2021.
Akizungumza katika kikao hicho, Lyimo amesema kuwa lengo la utafiti huo ni kuandaa mpango wa kurasimisha shughuli za waendesha bodaboda na bajaji ili wawe kwenye mfumo rasmi wa kuaminiwa kukopesheka na taasisi za fedha kuboresha maisha yao kiuchumi.
Lyimo amesema kuwa shughuli za urasimishaji wa vyombo hivyo, unaakisi dhana ya mpango wa Mkurabita wenye lengo la kuwawezesha wananchi kurasimisha rasilimali na biashara wanaomiliki na kuzitumia kama nyenzo ya kujiongezea kipato, mitaji na kupanua wigo wa ushiriki katika uchumi wa kisasa, unaoongozwa na sheria na kanuni za uchumi wa soko la ushindani.
Aidha, Lyimo amesema kuwa utafiti huo ulifanyika jijini Dodoma ni maandalizi ya uzinduzi wa urasimishaji wa shughuli hizo kwa nchi nzima ambapo wataanzia Makao Makuu ya Nchi Dodoma.
Naye, Afisa Urasimishaji na Uendelezaji Biashara wa MKURABITA, Zabron Makoye ameeleza jinsi utafiti ulivyofanywa na matokeo yake kuwa walianza kwa kukusanya dodoso za waendesha bodaboda/bajaji zilikusanywa kwa kwa kutumia simu janja na kwamba dodoso hizo zilitumika kupata taarifa za biashara.
Amesema kuwa uchambuzi wake ulilenga kupata taarifa za mahitaji halisi ya biashara hiyo ili kuwezesha timu ya urasimishaji kupanga vizuri mafunzo yaliyolenga kutatua changamoto ambazo wafanyabiashara walengwa wanakumbana nazo.
Meneja Urasimashaji Biashara wa MKURABITA,Hancy Kombe akichokoza mada wakati wa kikao hicho. |
Baadhi ya wadau wakiwa katika kikao hicho
Kikao kikendelea
Afisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) Dodoma, Ezekiel Emmanuel akichangia mada wakati wa kikao hicho.
Meneja Mauzo wa Kanda wa Benki ya NMB, Ungandeka Mwakatage akielezea kuhusu vigezo vya kukopa fedha kwenye benki hiyo.
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264204
Post a Comment