Na CCM Blog, Lumumba, leo
Wakati Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Uhuru Publications Ltd inayochapisha gazeti la Uhuru imewasimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Ernest Sungura, Mhariri Mkuu Ramadhani Mbwaduke na Msanifu wa kurasa Rashid Zahor, kwa kupotosha bahari kuhusu Rais Samia, Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo amesimamisha uchapaji wa gazeti la Uhuru kwa siku saba kuanzia leo.
Hatua hizo zimechukuliwa baada ya gazeti la Uhuru la leo Jumatano Agosti 11, 2021, kuandika katika habari Kuu katika Ukurasa wa kwanza kichwa cha Habari kwamba "SINA WAZO KUSANIA URAIS 2025-SAMIA", habari ambayo mbali na hatua zilizochukuliwa CCM imezikanusha, ikisema ni za upotoshaji.
" Kuhusu Swali ulilouliza kuwa Gazeti la Uhuru limeandika leo kichwa cha habari kinachopotosha kuhusu Rais Samia, na kwamba ni dalili ya mpasuku ndani ya CCM, nasema hiyo siyo kweli, bali ni kosa la kiutendaji ambalo ni suala la ndani.
Napenda nilizungumzie ingawa sikuwa nimedhamiria, kwanza mjue hili gazeti ni letu sisi Chama Cha Mapinduzi, kwa hiyo kosa lililofanyika ni kwamba tumemkosea sana Rais Samia Suluhu Hassan
Napenda kuchukua fursa hii kumuomba radhi kwa dhati kabisa Mwenyekiti wetu wa CCM Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna hii tuliyomkosea. Muungwana akifanya kosa ni vema kuomba radhi, tunamuomba radhi Rais Samia", alisema Chongolo na kuongeza;
"Sasa baada ya habari hiyo kutoka, niliiagiza Bodi ya Uhuru kukutana na ninadhukuru Bodi hiyo imekutana na kutoa maamuzi ya Kuwasimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu Ernest Sungura, Mhariri Mkuu Ramadhani Mbwaduke na Msanifu wa Kurasa Rashid Zahor.
Na mimi kwa nafasi yangu ya Ukatibu Mkuu wa Chama, nasimamishwa kuchapishwa gazeti la Uhuru kwa siku saba", alisema Chongolo.
Mapema akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, Chongolo ambaye alifuatana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Christina Mndeme na Katibu Mwenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka, Katibu Mkuu Chongolo alizungumzia pia mambo kadhaa.
Chongolo alizungumzia ziara ambayo yeye na Sekretarieti ameianza jana kwa kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Treni ya Mwendokasi (SGR) na pia leo smetembelea mradi wa ujenzi wa daraja la Salender.
Pia Katibu Mkuu, amesema Chama cha Mapinduzi kimeagiza Serikali kutoa fefha mapema kabla ya mwezi ujao kwa ajili ya miundombinu na huduma mbalimbali katika shuke za msingi na Sekondari.
Post a Comment