Kiongozi wa Maknisa Mkoa wa Dodoma, akiomba Mungu kufanikisha kikao hicho muhimu kwa viongozi wa dini na wengineo.
Mwakilishi wa Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, akiuombea dua mkutano huo. |
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Na Richard Mwaikenda, CCM Blog, Dodoma
Viongozi wa dini wameshauriwa kwenda kuwapatia waumini wao Elimu juu ya umuhimu wa chanjo ya Corona.
Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka wakati wa kuhitimisha kikao chake na viongozi alolihokiitisha kuwajengea uwezo kuhusu faida ya chanjo hiyo iliyozinduliwa jana mkoani humo.
Licha kikao hicho kuhudhuriwa na viongozi wa dini, kiliwashirikisha pia viongozi wa vyama vya siasa, mabaraza ya wazee na viongozi wa vyama vya watu wenye ulemavu kutoka Wilaya za Mkoa huo.
"Hatuwashawishi kwenda kupata chanjo, bali mnatakiwa muwapelekee waumini wenu elimu sahihi mliyoipata hapa kuhusu umuhimu wa chanjo hiyo ya Corona na kuwaacha waamue wenyewe kwa hiari kuchanjwa," amesema Rc Mtaka
Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Samuel Seseja aliwatoa hofu viongozi hao kuhusu usalama wa chanjo hiyo ya Corona ambapo pia alikiri kuwa madhira madodo madogo kama ilivyo hata kwa chanzo za magonjwa mengine.
Ili wapate uelewa mzuri wa kuweza kwenda kuwaelimisha waumini wao, viongozi walipata wasaa wa kuhoji mambo mbalimbali ikiwemo kutaka kujua ubora wa chanjo hiyo Janssen kutoka Marekani.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Fatma Mganga amewataka viongozi wa dini kuendelea kutoa maombi na toba kwa waumini ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya hilo la Corona.
Aidha, Dkt Mganga amesema kuwa katika mapambano dhidi ya janga hili la Corona inabidi kutumia silaha zote kupambana nalo ikiwemo kupigwa chanjo, maombi, lakini pia hawazuiwi kutumia tiba zingine walizozizoea kama vile kujifukiza,kutumia malimau, tangawizi na dawa zingine za asili zinazofaa.
Baada ya viongozi wengi kujiridhisha na elimu waliyoipata juu ya chanjo hiyo, walimuomba RC Mtaka kuwaandalia utaratibu wa kwenda kupata chanjo, ombi ambalo alilikubali.
Baadhi ya viongozi waliomba kupewa muda wa kwenda kuwaelimisha waumini wao juu ya elimu hiyo ya chanjo ya Corona.
Mkoa wa Dodoma umepata dozi 50,000 za chanjo ya Corona aina ya Janssen kutoka Marekani ambapo uzinduzi ulifanyika jana Julai 3,2021 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Makundi yaliyopewa kipaumbele ni wahudumu wa sekta ya afya, wazee wenye umri kuanzia miaka 50 pamoja na watu wenye magonjwa sugu kama vile pumu, athma, presha na kisukari.
Post a Comment