Featured

    Featured Posts

BALOZI WA ANGOLA AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA UONGOZI WENYE MAONO KWA TANZANIA NA WATU WAKE

 Na Bashir Nkoromo, CCM Blg

Balozi wa Angola hapa nchini Sandro de Oliveira, amempongeza Rais na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake aliosema ni wenye maono na wenye kuwajali Watanzania katika kufikia maendeleo ya kweli.


Balozi Sandro de Oliveira ametoa pongezi hizo alipokutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo, mazu.gumzo ambayo yamefanyika Ofisi kwa Katibu Mkuu huyo, katika Makao Makuu ya CCM Dodoma, leo.


Amesema Rais Samia tangu ashike hatamu ya Uongozi amekuwa akionyesha umahiri na dhamira ya dhati ya kulifikisha taifa la Tanzania kwenye mafanikio ya kiuchumi na kijamii huku akionyesha pia kuwa na maono chanya kwa Taifa.


Katika ziara hiyo ya kukutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo, Balozi Sandro de Oliveira aliambatana na mwakilishi wa Chama Tawala cha Angola MPLA Antonio Lobito.


Katibu Mkuu Chongolo na Balozi huyo katika mazungumzo yao walizungumza masuala mbalimbali ikiwemo yaliyolenga kuimarisha uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Angola, kindugu, kidiplomasia na Uchumi.


Pia walizungumzia kuendelea kukuza mahusiano ya kindugu uliodumu kwa miaka mingi baina ya Vyama vya Ukombozi vya CCM na MPLA uliojengwa na waasisi wa Mataifa hayo Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius  Nyerere na Hayati Agustino Netho.

Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Angola hapa Nchini Sandro de Oliveira, Ofisini kwake, Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma, leo.
Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Angola hapa Nchini Sandro de Oliveira, Ofisini kwake, Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma, leo. Wapili kushoto aliyeipa mgongo kamera ni mwakilishi wa Chama Tawala cha Angola MPLA Antonio Lobito.
Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo alipokuwa akimkaribisha Balozi wa Angola hapa Nchini Sandro de Oliveira, Ofisini kwake, Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma, leo. Nyuma ya Balozi huyo ni Mwakilishi wa Chama Tawala cha Angola MPLA Antonio Lobito.
Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Angola hapa Nchini Sandro de Oliveira (Kushoto) na Mwakilishi wa Chama Tawala cha Angola MPLA Antonio Lobito (kulia) wakati akiwasindikiza baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ofisini kwake, Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma, leo.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana