Featured

    Featured Posts

BUNGE LARIDHIA TANZANIA KUJIUNGA NA MKATABA WA ENEO HURU LA BIASHARA AFRIKA (AFCFTA)

 

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Profesa Kitila Mkumbo akiwasilisha Bungenii Jijini Dodoma azimio la kuanzisha eneo la mkataba huru la biashara Afrika kuwa ni pamoja na kupatikana kwa masoko mapya ya mazao ya kilimo na hivyo kuchochea uzalishaji wake. Mwenyekiti kamati ya kudumu ya Bunge, Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. David Kihenzile.

**************************

Serikali ya Tanzania imetaja baadhi ya faida za Bunge kuridhia Azimio la kuanzisha eneo la mkataba huru la biashara Afrika kuwa ni pamoja na kupatikana kwa masoko mapya ya mazao ya kilimo na hivyo kuchochea uzalishaji wake.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Profesa Kitila Mkumbo ameyasema hayo leo Alhamis Septemba 9 2021 bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha azimio hilo.

Mhe. Mkumbo metaja baadhi ya faida hizo kwa Tanzania ni pamoja na kuimarisha mnyororo wa thamani ya mazao ambayo mengi yanawahusisha wakulima wadogo.

“Kuongeza uzalishaji na ajira kwa wakulima na wadau wanaohusisha na mnyororo wa thamani wa mazao ya kilimo…Kupatikana na soko kubwa la bidhaa ,” amesema Mhe. Mkumbo.

Nyingine ni kuongezeka kwa uzalishaji kwa wakulima, ajira na thamani ya mazao ya kilimo.

Profesa Mkumbo ametaja faida nyingine ni kupatikana kwa soko kubwa la bidhaa na huduma lenye idadi ya watu takribani bilioni 1.2 ukilinganisha na idadi ya watu takribani milioni 522 katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Afrika Kusini mwa Afrika (SADC).

Pia kuongezeka kwa tija na ubora kwa bidhaa na huduma za Tanzania kutokana na kuongezeka kwa ushindani na hivyo kupelekea kupungua kwa bei za bidhaa.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana