Featured

    Featured Posts

CCM YAIAGIZA SERIKALI KUNUNUA TANI 100,000 ZA MAHINDI MIKOA YA MBEYA, SONGWE NA RUKWA

 


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo,akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 6,2021 jijini Dodoma.


Na CCM Blog Dodoma

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeiagiza Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa  Hifadhi ya Chakula (NFRA)  kununua tani 100,000 za mahindi katika Mikoa ya Nyanda za juu Kusini.

Hayo yamesemwa leo September 6,2021 jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa CCM,Daniel Chongolo wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa mwezi wa saba Sekretariet ya Chama cha Mapinguzi ilifanya ziara katika Mikoa ya Rukwa,Songwe na Mbeya ambapo walikutana na changamoto ya wakulima kukosa soko la zao la mahindi.

Amesema mara baada ya ziara hiyo waliiagiza Serikali kununua mahindi hayo ambapo  ilitoa zaidi ya shilingi bilioni 14 ambazo zilinunua zaidi ya tani 24,000.

”  kwa sasa fedha hizo zimeisha na wakulima wanaendelea kuhangaika kutafuta soko  la  kuuzia mahindi yao”amesema.

Chongolo ameiagiza Serikali kutoa tena fedha na inunue tani 100,000 za wakulima hao kwani wanazotaarifa kuwa  msimu ujao wa kilimo mvua zitakuwa chache.

“Tena kwa bei ile ile ya shilingi 500 kwa kilogramu na wafanye zoezi hilo liwe endelevu kwani mamlaka ya hali ya hewa imesema kuna changamoto katika mvua za vuli mpaka katika mvua za masika hivyo kutakuwa na changamoto ya upatikanaji wa chakula,”amesema Chongolo

Aidha Bw.Chongolo amesema katika ziara hiyo wamejifunza kwamba uchache wa vituo vya kununulia mahindi hivyo ameiagiza NFRA kuweka vituo ambavyo vitakuwa karibu na wakukulima.

“Kuna malalamiko kukatwa  fedha katika shilingi 500 tunasema hapana mtu aliyepo Mufindi,Ileje,Mbozi,Nkasi  tunataka bei ya mahindi iwe moja kwa wote wa karibu na mbali,”amesisitiza Chongolo.

Hata hivyo Chongolo ameziagiza  Wizara za Kilimo na Fedha na Mipango kukutana ili kujadiliana jinsi ya kupunguza bei ya mbolea kutokana na kuwa juu hivyo kumuumiza mkulima.

Amesema kwa sasa bei ya mbolea aina ya Urea imepanda maradufu kutokana na changamoto ya ugonjwa wa Corona ambapo awali ilikuwa shilingi 50,000 mpaka 55,000 lakini kwa sasa ni shilingi 80,000 mpaka 85,000.

“Tunaiagiza Serikali kupitia Wizara ya Kilimo na Wizara ya Fedha na Mipango waanze mchakato wa jinsi ya kuwasaidia wakulima.Nasisitiza Wizara zikutane mapema kuwezesha kupungua kwa bei ya mbolea,”amesema Chongolo

Pia Chongolo amesema kuwa mara baada ya maagizo hayo baada ya wiki mbili wataanza ziara ya kukagua maelekezo hayo.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana