Magazeti ya leo, gazeti la mwananchi, global publisher, habari leo, habari mpya, ippmedia,magazeti ya leo tanzania, magazeti ya udaku, michuzi, michuzi blog, mpekuzi huru, mwananchi, mwanaspoti,nipashe, sekretarieti ya ajira
Mbunge wa Ludewa, Joseph Kamonga akishiriki kuupokea Mwenge wa Uhuru katika Kata ya Mavanga ulipoanza kukimbizwa katika wilaya hizo ukitokea Mkoa wa Ruvuma Septemba 7, 2021.
Akizungumza katika eneo la mkesha katika Kata ya Mlangali baada ya kushiriki pia Mwenge ulipokuwa unazindua, unaweka mawe ya msingi na kukagua miradi, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuijali wilaya hiyo, kuipatia zaidi ya sh. milioni 30 ya kuendeleza ujenzi wa Barabara ya Njombe hadi Ludewa pamoja na fedha zingine ya ujenzi wa vituo afya na shule.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Marwa Rubirya (kulia) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru, Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Andrew Tsere tazari kuanza kukimbizwa wilayani humo baada ya kuupokea kutoka Mkoa wa Ruvuma Septemba 7, 2021.
Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru 2021, Luteni Josephine Mwambashi akiweka jiwe la msingi ujenzi wa Kituo cha Afya cha Shaurimoyo, Lugarawa.
Wananchi wa Kata ya Lugarawa, wakishangilia baada ya Mwenge wa Uhuru kuweka jiwe la Msingi ujenzi wa katika Kituo cha Afya Shaurimoyo.
Kamonga akizungumza jambo na Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Andrew Tsere alipokaribishwa kuzunguzya na wananchi wakati wa mkesha.
Mbunge Kamonga akiwasalimia wananchi katika eneo la mkesha katika Kata ya Mlangali.
Wanafunzi wakishangilia Mwenge wa Uhuru ulipowasiri eneo la mkesha katika Kata ya Mlangali.
Mwenge wa Uhuru ukikimbizwa katika Kitongoji cha Mkiu wilayani Ludewa.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Lugarawa wananchama wa Klabu ya kupinga rushwa wakiimba wakati Mwenge wa Uhuru ulipowasili shuleni hapo kuzindua klabu hiyo ambapo pia walimshukuru Mbunge wa Ludewa, Joseph Kamonga kuwapa ushirikiano wa hali na mali.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza/kuona kupitia clip hii ya video ujue yaliyojiri wakati wa mapokezi hayo......
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda Mhariri Blog ya Taifa ya CCM 0754264203
Post a Comment