Featured

    Featured Posts

KIONGOZI WA CCM USA SALMA MOSHI AMSAIDIA MAMA AMBAYE DAKTARI ALIMSHONA JERAHA NA KUMFUMUA MSHONO BAADA YA KUSHINDWA KULIPA 10,000 YA MATIBABU


Na Bashir Nkoromo, CCM Blog

Kiongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Marekani (USA) Salma Moshi ameguswa na kuamua kutoa msaada wa pesa kwa mkazi wa Kijiji cha Kerege Makaburini, Korogwe Vijijini, Zubeda Ngereza aliyepatwa na mkasa wa Daktari kumshona jeraha na kisha kumfumua mshono baada ya mama huyo kushindwa kulipa Sh. 10,000 ya matibabu katika Kituo cha Afya cha Kijiji hicho mkoani Tanga hivi karibuni..

"Nilipoiona hiyo 'story' kuhusu huyo mama, niliumia sana moyo, hivyo nikaamua kumtafuta, niliomba msaada wa namba yake kwa Kaka Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), akanitumia namba ya mtu mmoja aitwaye Kawoga ambaye ni ndugu yake na huyo mama.


Nikampigia Kawoga, nikamuomba nizungumze na huyo mama, nilipozungumz naye nikampa pole sana, nikamuomba kesho yake awe na Kawonga kwa Wakala, akafanya hiyo, ndipo baada ya kuzungumza na Wakala na huyo Mama na Kawonga nikatuma pesa, huyo mama akapewa hapohapo kwa Wakala", alisema Salma alipzungumza kwa simu na Mwandishi wa Blog hii ya Taifa ya CCM, leo.

"Kwa kweli Kaka yangu tukio alilofanyiwa huyu Mama ni baya na la kinyama, hivyo nilipolisikia niliumia sana moyo nikaona nitafute faraja kwa kujitolea kumsaidia pesa na baada ya mmi kufanya hivyo kuna Kiongozi mwingine wa CCM Uingereza ameniunga mkono, amesema na yeye atampatia pesa. ni tukio baya na la kuumiza lisiludiwe  tena, mama ameshukuru sana", alisema Salma huku akisema hawezi kutaja kiasi cha pesa alizotoa kwa sababu hakufanya hivyo kutafuta sifa bali amemtendea Mungu.

Kufuatia kadhia hiyo, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ilisema hivi karibuni kwamba video inayosambaa mitandaoni ikimuonyesha daktari aliyemshona jeraha mgonjwa na kufumua mshono kwa madai ya kushindwa kulipa gharama ni kweli, na kuthibitisha kuwa  tukio hilo lilitokea Julai, 2021

Ofisi hiyo imesema ni kweli lilitokea katika kituo cha afya Kerenge kilichopo tarafa ya Magoma Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.

Ofisi hiyo ilitoa maelezo hayo Jumamosi Septemba 4, 2021 baada ya kusambaa mitandaoni kwa video ya tukio hilo na kuzua mjadala mtandaoni huku Wizara ya Afya ikitoa tamko na kuomba mwenye kufahamu eneo husika kutoa taarifa na kisha kuweka namba ya simu.

Naibu Katibu Mkuu Tamisemi anayeshughulikia afya, Dk Grace Magembe akamtaja mtumishi aliyekiuka miiko ya udaktari kwa kuhusika na tukio hilo kuwa ni Dk Jackson Meli ambaye ni ofisa wa Kituo cha Afya cha Kerege ambacho ni cha umma.

“Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ameshachukua hatua kwa kumsimamisha kazi na amempa hati ya mashtaka na pia ameshafikishwa kwenye Baraza la Madaktari ili achukuliwe hatua stahiki kwa kwenda kinyume na miiko ya taaluma ya udaktari,” akasema Dk. Magembe.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Korogwe, Mkoa wa Tanga, Halfani Magani tayari amemsimamisha kazi Tabibu wa Zahanati ya Kerenge, Jackson Meli baada ya kufumua mshono wa mgonjwa  Zubeda Ngereza kufuatia mgonjwa huyo kushindwa kulipa pesa za matibabu kiasi cha Tsh 10,000.

Magani amesema mtuhumiwa huyo ambaye tayari amekamatwa na Polisi kwa ajili kumhoji na uchunguzi, atafikishwa Mahakamani kwa kosa la kukiuka maadili ya utabibu na kanuni za utumishi wa umma.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana