MBUNGE wa Ludewa, Joseph Kamonga na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ludewa, Bakari Mfaume wakikagua ujenzi wa kipande cha Barabara kuu ya kutoka Njombe kwenda wilayani humo na kujiridhisha na maendeleo yake.
Kamonga akipata maelezo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa barabara |
MBUNGE wa Ludewa, Joseph Kamonga na Mwenzekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaza ya Ludewa, wamekagua ujenzi wa kipande cha Barabara kuu ya kutoka Njombe kwenda wilayani humo na kujiridhisha na maendeleo yake.
Akizungumza alipofika katika eneo la ujenzi akitokea Bungeni Dodoma jana, Kamonga amesema kuwa licha ya ujenzi wa barabara hiyo inayojengwa kwa zege kuchukua muda mrefu lakini sasa ujenzi wake unakwenda vizuri, unaridhisha.
"Mwenendo si mbaya kazi inaendelea vizuri, KM. 50 tayari ujenzi wake umekamilika bado Km 50 nyingine na kwamba baada ya serikali kutoa sh. bil. 30, Km nyingine 30 zinaendelea itakuwa bado sh. Bil. 20 kukamilisha Km. 100," amesema Kamonga.
Kamonga amesema kuwa fedha hizo sh. Bil. 30 zimetolewa baada ya hivi karibuni Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi, Godfrey Msongole na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dkt. Bernard Chamuriho kukagua ujenzi wa barabara hiyo unaofanywa na Kampuni ya Korea Kusini, Choan Kwong.
Ameyasema hayo walipokutana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ludewa, Bakari Mfaume na kwa pamoja kukagua berabara hiyo eneo la Lubonde ambapo waliwakuta wafanyakazi wa Kampuni hiyo, wakiendelea na kazi.
Akizungumza na viongozi wa Kampuni hiyo, Mhandisi Mkazi wa Kampuni hiyo, Deng Ryeol na Mhandisi wa Vifaa vza Ujenzi, Heemin Park waliwahakikishia kuwa pasingekuwa na mvua zinazo karibia kuanza hivi karibuni wangemaliza ujenzi Desemba mwaka huu, lakini sasa ujenzi wake utakamilika Julai mwakani.
Naye Katibu wa CCM Wilaza ya Ludewa, Mfaume ameishukuru Serikali ya Awamu ya 6 inazoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea barabara hiyo muhimu ambayo hivi sasa ujenzi wake unaendelea vizuri na kwamba ikikamilika itawaletea unafuu wananchi wa wilaya hiyo.
Post a Comment