Tegeta, Dar es Salaam
Kanisa Halisi la Mungu Baba linatarajiwa kutikisa mji wa Sumbawanga mkoani Rukwa wakati ibada kubwa mno na ya aina ya kipekee iliyoandaliwa na Kanisa hilo itakaporindima katika mji huo, Jumapili hii, Septemba 12, 2021 (26 Tamuzi).
Baba Halisi wa Uzao wa Kanisa hilo lenye Makao yake Makuu Tegeta jijini Dar es Salaam, amesema, ibada hiyo itafanyika katika Ukumbi wa Boma, jirani na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya katika mji huo wa Sumbawanga.
Amesema maandalizi yamekamilika na amewaomba wakazi wa mji huo wa Sumbawanga na maeneo jirani na hata wa mikoa jirani kuhudhuria kwa wingi kwenye ibada hiyo kwa kuwa itakuwa ni ibada ambayo hawajapa kuiona.
Baba Halisi wa Uzao amesema, ibada hiyo itaanza kurindima mda wa saa 8 mchana hadi saa 10 jioni.
"Ujumbe wa Ibada hiyo utakuwa ni 'Kuweka taa juu ya kiango wapate kuiona nuru yake Luka 8:16 Marko 8:16' ", Baba Halisi amebainisha.
Post a Comment