Featured

    Featured Posts

KATIBU MKUU WA CCM DANIEL CHONGOLO KUANZA KESHO ZIARA YA SIKU 7 MIKOA YA KUSINI NA NJOMBE

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog Dar

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo kesho anaaza ziara ya kikazi ya siku 7 katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Njombe akiambatana na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.

Taarifa iliyotolewa na Makao Makuu ya CCM, Dodoma, imesema ziara hiyo itaanzia katika Wilaya zote za mkoa wa Lindi na kuemdelea katika mikoa ya Mtwara na Ruvum na kuishia katika mkoa wa Njombe Septemba 21, 2021.

"Malengo ya ziara hiyo ni kuimarisha Uhai wa Chama katika ngazi za Mashina pamoja na Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 – 2025, ikiwa ni Utekelezaji wa Maelekezo ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kilichofanyika tarehe 29 Juni, 2021", imesema Taarifa hiyo.

Taarifa imewataja Wajumbe wa Sekretarieti watakaoshirikia katika ziara hiyo kuwa ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM – Bara Christina Mndeme, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ngemela Lubinga.

 

Wengine ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Kennan Kihongosi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania Dk. Philis Nyimbi na Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Gilbert Kalima.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana